WANANCHI KUJIANDIKISHA DAFTARI WAPIGA KURA
Na Charles Mariagorreth
Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Bagamoyo Ndg.Shauri Selenda amewataka Wananchi na Wakazi wote wa Jimbo la Bagamoyo kujitokeza kujiandikisha kwenye Daftari la kudumu la Mpiga kura awamu ya pili.
Afisa Mwandikishaji wa jimbo Hilo ametoa wito huo kupitia kupindi cha Redio Morning Packege ya Harvest Times fm 100.1 na kusema kuwa wananchi watumie fursa hii kujiandikisha ili kuwa na vigezo husika vya kumwezesha kupiga kura ifikapo mwezi Oktoba 2025.
Hata hivyo Ndugu Shauri amesisitiza kuwa umri wa kujiandikisha lazima uwe umetimiza miaka 18 na zaidi na kuwa raia wa Tanzania.
Aidha ,Afisa Mwandikishaji amewataka wale ambao tayari wamejiandikisha kwa awamu ya kwanza na kupatiwa vitambulisho vyao vya mpiga kura wanatakiwa kwenda kuhakiki taarifa zao kwenye vituo walivyojiandikisha hapo awali.
Zoezi la uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura awamu ya pili linatarajiwa kuanza hapo kesho tarehe 16 Mei hadi 22 Mei 2025. Hivyo wananchi wamezidi kuaswa kutumia fursa hii kama kibali Cha kuweza kupiga kura na ikiwa kama haki ya kila Mtanzania mwenye sifa za kupiga kura.
Comments
Post a Comment